Majaji wakiwa kazini katika Shindano lililofanyika Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza.Picha na Maktaba.
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions, Dar Es Salaam
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Kwa KAnda ya Pwani limemalizika leo Mkoani Dar Es Salaam mara baada ya washindi watano watakaoiwakilisha Kanda hii katika Fainali kubwa itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa nane kupatikana katika Ukumbi wa Makumbusho na hatimaye washindi hao Kukabidhiwa shilingi laki tano taslimu.
Shindano hili lilianza tarehe 30 Mei 2014
na kusimama kwa Muda kutokana na Msiba wa George Tyson ambae alikuwa ni mzazi mwenza wa jaji Yvonne Cherry au Monalisa. Katika Kuungana nae katika kipindi kigumu alichopitia Timu nzima ya TMT ilibidi kusimamisha Shindao hilo Kwa Muda hadi pale Msiba kumalizika, na Baada ya Msiba kumalizika Shindano hili liliendelea tena mnamo tarehe 15 June 2014 na kufikia tamati leo kwa Washindi watano Kupatikana.
na kusimama kwa Muda kutokana na Msiba wa George Tyson ambae alikuwa ni mzazi mwenza wa jaji Yvonne Cherry au Monalisa. Katika Kuungana nae katika kipindi kigumu alichopitia Timu nzima ya TMT ilibidi kusimamisha Shindao hilo Kwa Muda hadi pale Msiba kumalizika, na Baada ya Msiba kumalizika Shindano hili liliendelea tena mnamo tarehe 15 June 2014 na kufikia tamati leo kwa Washindi watano Kupatikana.
Kanda ya Pwani inahusisha Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar Es Salaam ambapo takribani washiriki 300 waliweza kujitokeza kwaajili ya kushiriki shindano hili kwa Kanda ya Pwani.
Washindi watano waliopatikana katika Kanda ya Pwani wataungana na Washindi wengine kutoka Kanda ya Ziwa, Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kusini na Kaskazini ambao walishapatikana kwaajili ya kuingia kambini ambapo wawakilishi hao wa kanda hizo watapewa mafunzo kutoka Kwa Walimu wa Sanaa wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam na Kutoka Chuo Cha Sanaa cha Bagamoyo na hatimaye wataendelea na mchujo ambapo Mshindi mmoja ataondoka na Kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika fainali kubwa itakayofanyika mwisho wa Mwezi wa nane.
Vilevile vipindi vya Shindano hili vinarushwa katika kituo cha runinga cha ITV siku ya Jumamosi saa 4 Usiku na Marudio yake ni Saa 10 Jioni siku ya Jumapili na Jumatano ni saa 5 usiku.
Na Jumamosi ya Wiki kipindi cha Dar Es Salaam kitarushwa muda ule ule wa Saa 4 Usiku siku ya Jumamosi na marudio yake siku ya Jumapili saa 10 Jioni na Jumatano saa 5 usiku.
Washindi wa Kanda zote wanatarajia kuwasili katika Nyumba ya TMT hivi karibuni kwaajili ya Kuanza kambi kwaajili ya safari ya kuwania Shilingi Milioni 50 katika fainali kubwa itakayofanyika mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
Vilevile katika Fainali hiyo washindi kumi bora watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions ambao ni waandaaji na waendeshaji wa Shindano hili na hatimaye wataweza kufanya kazi ya pamoja na hatimaye kunufaika na Kazi hiyo.
Shindano hili la Tanzania Movie Talents (TMT) lilianza safari zake za kusaka Vipaji katika Kanda ya Ziwa na kuendelea na zoezi hilo kanda ya Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kusini na Kaskazini na hatimaye safari hizo zimefikia tamati leo mara baada ya washindi watano kupatikana kutoka Kanda ya Pwani.
No comments:
Post a Comment