Bondia
wa ngumi za kulipwa anayeshikilia mkanda wa WBF, Francis Cheka,
amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro,
akikabiliwa na shtaka la shambulio la kudhuru mwili na kujeruhi.
Cheka
amefikishwa leo kwa mara ya kwanza katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa
wa Morogoro, na kusomewa shtaka, na mwendesha mashtaka wa polisi,
Aminata Mazengo, mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Said Msuya, akidaiwa
mnamo julai 02 mwaka huu, bila halali na akijua kufanya hivyo ni kosa
kisheria, amempiga kwa ngumi maeneo ya kichwani na tumboni, Bahati
Kabanda maarufu kama Masika, na kumsababishia maumivu makali.
Cheka
anadaiwa kutenda kosa hilo kwa kabanda ambaye alikuwa ni meneja wa baa
yake ya Vijana Social iliyopo sabasaba katika manispaa ya Morogoro baada
ya kudaiwa kutoridhishwa na mahesabu ya mauzo, ambapo mahakama ilitoa
masharti ya dhamana, ikimtaka kuwa na wadhamini wawili kwa kila mmoja
kuweka dhamana ya maandishi ya shilingi milioni moja, ama aende rumande,
ambapo hadi ITV inaondoka mahakamani hapo, taratibu za dhamana zilikuwa
zikiendelea.
Source:ITV
No comments:
Post a Comment