Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, July 28, 2014

DAKTARI AFARIKI KWA EBOLA


Idara ya afya nchini Liberia imetangaza kuwa Daktari mmoja wa Ebola amefariki kutokana na viini vya ugonjwa huo.

Ni daktari wa kwanza nchini humo kufariki kutokana na ugonjwa huo tangu uzuke mapema mwaka huu.

Daktari Samuel Brisbane aliambukizwa viini vya 

ugonjwa huo alipokuwa akiwatibu wagonjwa wa Ebola katika mji mkuu wa Monrovia.

Alihudumu kama daktari wa watu wengi maarufu akiwemo rais wa zamani Charles Taylor.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa takriban watu 660 wamethibitishwa ama wanashukiwa kufariki na ugonjwa huo Magharibi mwa Afrika tangu mwezi February na kuufanya kuwa ugonjwa m'baya zaidi tangu uzuke.

No comments:

Post a Comment