FIFA imeipiga marufuku Nigeria
Nigeria imepigwa marufuku ya kushiriki mashindano yeyote ya
kandanda yanayoandaliwa na shirikisho la soka duniani FIFA.
Hatua hii imeafikiwa baada ya maafisa wa serikali kuwaondoa
wasimamizi wa shirikisho la soka nchini Nigeria NFF afisini.
Marufuku hii inamaanisha hakuna klabu yeyoye ya soka nchini
Nigeria inaweza kushiriki mashindano yeyote ya Kimataifa.
FIFA ilikuwa imeionya Nigeria kuwa ingeichukulia hatua
ifikiapo Jumanne kama Shirikisho la NFF halijarejeshewa madaraka yao lakini
Serikali ikapuuza makataa hayo.
Mwishoni mwa juma Serikali ya Nigeria ilikuwa imemteua afisa
mshikilizi kuongoza shirikisho hilo hadi uchaguzi wa huru na wa haki
utakapofanyika kulingana na taarifa ya wizara ya michezo.
FIFA katika taarifa imeonya kuwa marufuku hiyo itaondolewa
tu iwapo maafisa waliochaguliwa watarejeshwa mamlakani.
Marufuku hiyo itaathiri timu ya taifa ya Super Eaglets ya
wasichana wasiozidi umri wa miaka 20 ambayo inapaswa kushiriki mchuano wa kombe
la dunia iwapo marufuku hiyo haitaondolewa ifikapo juma lijalo.(Julai15)
Msemaji wa serikali hata hivyo alisema kuwa hatua
iliyochukuliwa dhidi ya NFF ilifuata kanuni kwani hata kiongozi wa shirikisho
la soka la Nigeria Aminu Maigari alikamatwa na polisi punde baada ya kurejea
nyumbani kutoka Brazil.
Mahakama ya Nigeria ilikuwa imeamua kuwa Maigiri hakuwa
anastahili kuendelea kuiongoza NFF haswa baada ya matokeo duni huko Brazil.
Wajumbe wa NFF waliafiki kauli ya mahakama ya kumn'goa
mwenyekiti huo madarakani lakini lakini kwa sasa erikali ya Nigeria inasubiri
mawasiliano kutoka FIFA baada ya kutuma ithibati ya mkutano maalum uliofanyika
na wajumbe wa shirikisho la soka la NFF .
Mabingwa hao wa Afrika walishindwa katika mkondo wa pili wa
kombe la dunia na Ufaransa .
Hiyo ilikuwa ni mara ya tatu kwa timu hiyo kufuzu kwa mkondo
wa pili baada ya kufuzu mwaka wa 1994 na 1998.


No comments:
Post a Comment