Miili ya marehemu ikiwa katika eneo la dharura katika
hospitali ya mkoa wa shinyanga
Hapa ni katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa
Shinyanga ambapo majeruhi 29 hadi sasa wamepokelewa kufuatia ajali ya gari aina
ya fuso iliyokuwa imebeba watu wengi pamoja na mizigo kuelekea katika mnada wa
Mhunze uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.Ajali hiyo imetokea asubuhi ya
leo Alhamis.Pichani majeruhi waliendelea kuhudumiwa na wataalam wa afya katika
hospotali ya mkoa wa Shinyanga
Kwa mujibu wa kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel ameiambia malunde1 blog kuwa mpaka sasa wamepokea miili miwili ya marehemu na majeruhi 29 |
Huduma inaendelea kutolewa katika hospitali ya mkoa wa
Shinyanga
|
Baadhi ya majeruhi wameiambia blog Hii kuwa gari aina ya
fuso waliyokuwa wamepanda tena kwa kujazana ilikuwa inafukuzana na fuso
nyingine na ghafla walijikuta wakiwa wameshapinduka
Kulia ni kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa
Shinyanga Dkt Maguja Daniel akichukua maelezo kutoka kwa askari wa usalama
barabarani
|
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt
Maguja Daniel akizungumza na waandishi wa habari hivi punde-Picha zote na
Kadama Malunde-Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment