TANGAZO
JESHI LA KUJENGA TAIFA, LINAKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA
KWA KUTUMIA UJUMBE MFUPI WA MANENO (SMS) KATIKA SIMU ZA VIGANJANI NA MTANDAO WA
JAMIIFORUM.COM, KWAMBA VIJANA WA KUJITOLEA NA MUJIBU WA SHERIA WANAOENDELEA NA
MAFUNZO KATIKA MAKAMBI YA JKT WANAKUFA KWA UKATILI, WAKITOLEA MFANO KAMBI YA
JKT OLJORO ARUSHA KWAMBA KUNA VIJANA WATATU WAMEFARIKI DUNIA.UMMA UFAHAMU KUWA
TAARIFA HIZO SI ZA KWELI NI UPOTOSHAJI KWA VIJANA NA WATANZANIA. UKWELI NI
KWAMBA KUNA KIJANA MMOJA WA KIKE HONORATA VALLENTINE OISO ALIYEFARIKI KATIKA
KIKOSI CHA JKT OLJORO ARUSHA KWA UGONJWA WA UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIA)
ULIOSABABISHWA NA MALARIA.
SIO VIJANA WATATU KAMA INAVYOELEZWA KWENYE UJUMBE
UNAOSAMBAZWA. WAZAZI WA KIJANA ALIYEFARIKI PIA WALITHIBITISHA KUWA KIJANA WAO
ALIKUWA NA MATATIZO YA UPUNGUFU WA DAMU.
JESHI LA KUJENGA TAIFA LINASISITIZA KUWA HAKUNA UKATILI
WOWOTE UNAOFANYWA KWA VIJANA WANAOENDELEA NA MAFUNZO KATIKA MAKAMBI YA JKT.
JKT LINALAANI KITENDO HICHO NA LINAFUATILIA ILI KUBAINI
CHANZO CHAKE. MTU YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUWA NDIYE CHANZO CHA UJUMBE HUO, HATUA
ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.JESHI LA KUJENGA TAIFA LINAWAKUMBUSHA
VIJANA NA WATANZANIA KUWA MAKINI NA MATUMIZI MABAYA YA SIMU ZA MIKONONI NA
MITANDAO YA JAMII, HASA KWA TAARIFA ZINAZOHUSISHA JESHI.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MAKAO MAKUU YA JKT
No comments:
Post a Comment