Mwanamuziki maarufu wa Marekani Justin Bieber amekiri kosa
la kufanya uharibifu katika nyumba ya jirani yake.
Mahakama imemtaka alipe faini ya dola 80,900 na pia kufanya
kazi ya jamii kwa muda wa miaka mitano.
Wapelelezi walifanya msako kwa nyumba ya Bieber huko
Calabasas Carlifonia wakitafuta ushahidi uliompelekea kusababisha uharibifu huo
na baada ya msako huo rafiki mmoja wa Bieber alipatikana na mihadarati na
kunaswa.Kwa mujibu wa polisi, ushahidi huo wa video ulionaswa nyumbani mwa
Bieber ulionyesha Bieber akiwasalimu maswahiba wake baada ya kurusha Mayai kwa
nyumba ya jirani yake na kusababisha uharibifu.Mashtaka ya Bieber yangewekuwa
mabaya zaidi iwapo uharibifu huo ungesababisha hasara inayozidi dola elfu
ishirini.
Bieber atawekwa chini ya uangalizi wa polisi kwa muda wa
miaka miwili na iwapo ataonyesha mabadiliko atawachwa huru.Mahakama pia ilitoa
uamuzi kuwa Bieber apate mafunzo ya kudhibiti hasira, kikamilifu. Bieber ambaye
anakabiliwa na mashtaka mengine mawili ya uhalifu huko Florida na Toronto,
hakufika mahakamani uamuzi huu ulipotolewa.
Mawakili wake walisema kuwa Bieber amefurahi kuwa jambo hilo
limesuluhishwa na ataendelea kusonga mbele na kuwa makini katika kazi yake ya
muziki.
Tangu kisa hiki Bieber alihamia Beverly Hills kutoka
Calabasas.
Uchunguzi wa hapo awali uliojaribu kufuatilia tabia za
Bieber haukumpata Bieber na makosa ambayo yangepelekea kumfungulia mashtaka
yoyote.Waendesha mashtaka mahakamani walikana kumfungulia mashtaka mwaka
uliopita baada ya jirani yake kulalamika kuwa mwezi Novemba 2012 Bieber
aliendesha gari bila kujali na kupita eneo asilopaswa.
Hayo yakijiri, Bieber pia alishtakiwa huko Miami kwa
kuendesha gari akiwa mlevi na bila lessen halali. Kesi hiyo itasikilizwa
baadaye mwezi huu. Aidha, katika msururu huo wa kesi, Bieber ameshtakiwa
kushambulia dereva mmoja mnamo mwezi Disemba huko Toronto.



No comments:
Post a Comment