Mkuu
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, (ZCO),
Jafar Ibrahim, (Kulia), akizungumza na Mwanasheria wa kampuni ya The
Guardian, Gladis Frimbari (Wapili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa The
Guardian, Kiondo Mshana, (Wa pili kushoto) na Mhariri Mtendaji wa
Nipashe, Jesse Kwayu, (Wa kwanza kushoto), ofisini kwake jijini.
Kachero huyo aliwaomba radhi viongozi hao wa The Guardian, kutokana na
makosa ya kuwaita polisi kwa mahojiano kuhusiana na habari
iliyochapishwa na Nipashe ikiwahusisha polisi wa pikipiki na vitendo vya
rushwa, na kwamba Polisi haina tatizo na habari hiyo. (Picha kwa Hisani ya The Guardian)
Mkurugenzi
Mtendaji wa The Guardian Limited, Kiondo Mshana, (Katikati), Mhariri
Mtendaji wa Nipashe, Jesse Kwayu, wakiwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa
Upelelezi Makosa ya Jinai, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ZCO, Jafar
Ibrahim jijini. Hata hivyo
Mkuu huyo wa upelelezi, aliomba radhi kwa vile wito huo ulitolewa kimakosa, ukiwataka wakuu hao kufika polisi kwa mahojiano kuhusu habari iliyochapishwa na Nipashe, ikiwahusisha polisi wa pikipiki na ulaji rushwa.
Mkuu huyo wa upelelezi, aliomba radhi kwa vile wito huo ulitolewa kimakosa, ukiwataka wakuu hao kufika polisi kwa mahojiano kuhusu habari iliyochapishwa na Nipashe, ikiwahusisha polisi wa pikipiki na ulaji rushwa.
RAMADHANI TEMBO
NA ZAWADI CHOGOGWE
ASKARI wa
Jeshi la Polisi Kikosi cha Pikipiki
(Tigo), wamezua sintofahamu baada ya wananchi kutoa malalamiko yao juu
ya askari hao kuonekana sehemu
mbalimbali wakikamata magari na Pikipiki na kudaiwa kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa madereva .
Wananchi wamekuwa wakilalamika juu ya askari hao
kuhusika kuomba na kupokea rushwa na kuvunja sheria
za Jeshi hilo na kulidhalilisha na kushindwa kuwajibika katika kulinda
usalama wa raia na mali zao.
Kutokana na
malalamiko hayo, gazeti la Nipashe liliandika kuhusiana na malalamiko hayo
katika toleo la Julai 8, mwaka huu
katika ukurasa wa kwanza, gazeti hilo
lilieleza matukio mbalimbali yanayofanywa na kikosi hicho huku wakiliomba Jeshi
la Polisi kulifanyia kazi suala hilo.
Kutolewa kwa taarifa hiyo, Jeshi hilo
mnamo Julai 21 mwaka huu lilituma
barua ya wito kwa Mhariri
Mtendaji wa gazeti hilo, Jesse
Kwayu iliyomtaka afike jana saa
nne asubuhi Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano
kuhusiana na toleo hilo.
Baada ya
kupata barua hiyo, Mkurugenzi wa gazeti hilo, Kiondo Mshana akiongozana na
Mhariri mtendaji Jesse Kwayu pamoja na mwanasheria wao Gladiys Fimbari , waliitikia wito huo na kufika ofisini hapo kwa
ajili ya mahojiano hayo.
Kabla ya
kuanza kwa mahojiano hayo, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi ambaye pia ni
Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jafari Mohamed,alisema kuwa
barua hiyo iliandikwa kimakosa kwa kuwa hakuna tuhuma zozote kuhusiana na toleo
lililotolewa na gazeti hilo.
Alisema kuwa
lengo la barua hiyo ilikuwa ni kutaka ufafanuzi dhidi ya malalamiko ya Wananchi yanayohusiana na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa
vinavyofanywa na kikosi hicho.
“Tunawaomba
radhi kwa usumbufu uliyojitokeza na kuacha majukumu yenu ya kazi na suala hili
litashugulikiwa na ofisi na kuwachukulia hatua za kisheria askari hao”alisema.
Kwa upande
wake Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo alisema kuwa kutokana na utendaji mbovu wa
askari hao iliwalazimu waandike taarifa hizo, lakini cha kushangaza Julai 21
walipata barua hiyo inayowataka wafike kwa mahojiano na baada ya kufika hapo
ilionekana barua hiyo imekosewa,hivyo wamekubali kuombwa radhi na
watashiriakiana na Jeshi hilo kutoa taarifa zozote za uhalifu.
No comments:
Post a Comment