Mmoja wa watuhumiwa wa matukio ya ugaidi nchini Kenya,Jihad
Gaibon Swaleh, amefikishwa mahakamani nchini Tanzania.Mshukiwa huyo amesomewa
mashtaka ya kufadhili vitendo vya kigaidi nchini Kenya.Pamoja naye watuhumiwa
wengine 16 ambao wanadaiwa kuendesha vitendo vya kigaidi nchini Tanzania pia
wamefikishwa mahakamani hii leo wakikabiliwa na tuhuma za kula njama ya kutenda
makosa ya kigaidi nchini Tanzania.
Washtakiwa wote 17
wamerejeshwa rumande baada ya kusomewa
mashtaka ya vitendo vya kigadi nchini Tanzania pamoja na nchi jirani ya Kenya.Upande
wa mashtaka ukiongozwa na mwendesha mashtaka ambaye ni wakili wa serikali
mwandamizi Prosper Mwangamila ulidai mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es Salaam, kuwa kwa kutumia mtandao wa facebook aliweza kushawishi
watu wengine kuwasiliana kwa lengo la kutafuta vifaa vya kulipua mabomu nchini
Kenya na kusababisha majerahi, hofu na Vifo.
Jihand Gaibon Swaleh ambaye amesomewa mashtaka mawili
hakuruhusiwa kukiri wala kukana mashitaka yanayomkabili kutokana na kwamba
mashitaka hayo yanaangukia katika makosa ya ugaidi ambayo kwa mujibu wa sheria
nchini Tanzania mahakama ya Hakimu Mkazi haina mamlaka ya kuendesha kesi za
namna hiyo.
Katika kesi ya awali kutajwa mahakamani hapo washtakiwa
wengine 16 walisomewa mashtaka mawili ikiwemo kula njama kutenda kosa pamoja na
kushawishi wenzao kushiriki katika vitendo vya kigaidi katika sehemu mbali
mbali nchini Tanzania.
Ni makosa ambayo wanadaiwa kutenda kati ya Januari mwaka
2013 na Juni 2014 katika maeneo tofauti Tanzania.Katika kesi zote mbili dhidi
ya washtakiwa hao Upande wa mashtaka uliiambia mahakama iliyokuwa chini ya
hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo bi Hellen Riwa kuwa upelelezi bado unaendelea
na hivyo kuiomba mahakama kuahirisha kesi hizo hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Julai.
Awali mapema asubuhi msemaji wa jeshi la polisi nchini
Tanzania Bi Advera John Bulimba aliwealeza waandishi wa habari kuhusu tuhuma
dhidi ya washtakiwa hao
Hii ni mara ya kwanza kwa kundi kubwa la watuhumiwa
kufikishwa mahakamani kwa pamoja wakikabiliwa na tuhuma za makosa ya kigaidi
huku mtandao wa kijamii wa facebook nao ukitajwa kuhusika katika kutawanya
taarifa za kuwezesha kutenda makosa hayo.CHANZO BBC


No comments:
Post a Comment