Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, July 10, 2014

ORIGI MAMBO SAFI KWA MAJOGOO WA JIJI, MUDA WOWOTE ANAMWAGA WINO!



Divock Origi (kulia) amesafiri mpaka Liverpool kujadili uwezekano wa kujiunga na klabu hiyo.
Liverpool wanakaribia kukamilisha usajili wa wachezaji wawili, nyota wa Ubelgiji katika fainali za kombe la dunia mwaka huu, Divock Origi na winga wa  Benfica, Lazar Markovic.
Usajili huo utaigharimu Liverpool dau la paundi milioni 30.
Orig alipigwa picha akiwasili mjini Liverpool jana jumatano ili kuzungumza na maofisa wa klabu katika uwanjani wa mazoezi wa Melwood na anaweza kupimwa afya  leo alhamisi.
Ada ya uhamisho ya paundi milioni 19.8 kwa ajili ya Markovic inaaminika imeshakubaliwa na Benfica, wakati Origi anaonekana ataigharimu Liverpool paundi milioni 10 kutokea klabu ya Lille ya Ufaransa,.
Hata hivyo, nao Tottenham waliripotiwa kuiwinda saini ya nyota huyo


Origi (pichani mwenye nguo yenye rangi ya njano) alichukuliwa kwenda uwanja wa mazoezi wa Liverpool, Melwood

No comments:

Post a Comment