Kampuni ya uwindaji ya Gree Miles Safari Limited(GMS) iliyokuwa ikifanya kazi zake za uwindaji Tanzania ilifutiwa leseni yake rasmi wiki iliyopita kutokana na kampuni hiyo kwenda kinyume na makubaliano na sheria za uwindaji za Tanzania.
Ilifika wakati ambapo kampuni hiyo ilithubutu kuwinda hadi ndege wakati ilikuwa hajaruhusiwa ama kukubaliana na serekali ya Tanzania kufanya hivyo.
Vibaya zaidi kampuni hiyo ilianza hata kukamata wanyama wadogo na kuwachukua wakati hilo pia halikuwa ndani ya makubaliano yake na serekali.
Hata hivyo, baada ya waziri Nyalandu kuifutia leseni, kampuni hiyo iliruhusiwa kufungua mashtaka mahakamani kutokana na hasara ambayo itakuwa imesababishiwa ili sheria ichukue mkondo wake kama itaona kuwa imeonewa kwa kitendo hicho.
Angalia picha zake hapo chini ili upate kuona shughuli za kampuni hiyo kwa ujumla pamoja uvunjifu wa sheria na makubaliano yake na serekali ya Tanzania:
|
Kampuni hiyo ikiwinda ndege |
|
kampuni ya GMS ikiwa imekamata ndege |
|
Ikiwa imemkamata mnyama mdogo kwa lengo la kumbeba |
|
Ikiwa imemkamata mnyama kwa lengo la kuondoka naye
|
|
Wawindaji wa GMS wakiwa wamemkamata ndege |
|
Hapa wawindaji wa GMS wanampakia mnyama waliokwisha kumuua kwenye gari |
|
Mnyama aliyejeruhiliwa kwa risasi. Anamaliziwa kwa risasi nyingine hapa chini: |
|
aliyekwisha kuuawa kwa risasi, tayari kuchukuliwa |
|
Wawindaji wakiwa mawindoni |
|
Wawindaki wakimpakia nyama waliyemuua |
|
Mnyama aliyeuawa, tayari kwa kusafirishwa |
Sasa swali langu ni je, mpaka muda huu serekali inaposhtuka kuwa wawindaji hawa wanavunja sheria ni kwa kiasi gani Tanzania imepata hasara kubwa?
Na je, ina maana kuwa watanzania wameshindwa hata kuwa na makampuni ya uwindaji mpaka kuyasajili makampuni ya wageni ambao hawana uchungu na taifa letu?CHANZO BLOGU YA WANAINCHI
No comments:
Post a Comment