Basi la wachezaji wa soka TZ lakamatwa ili kulipa madeni
Basi la wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, limekamatwa
kwa amri ya mahakama kutokana na deni la shilingi milioni 140 (zaidi ya dola
85,000), ambalo kampuni ya Punchline kutoka Kenya, inadaiwa kulidai shirikisho
la kabumbu Tanzania (TFF).
Madalali ndiyo walilikamata basi hilo likiwa kama
dhamana
huku TFF ikitakiwa kulipa deni husika kabla ya kurejeshewa mali zao.
Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface
Wambura, amesema tayari wamelipa shilingi millioni 70 ikiwa ni malipo ya awali.
Deni hilo linatokana na gharama za uchapishaji tiketi za
kuingilia uwanjani katika mechi za ligi kuu ya Tanzania tangu mwaka 1997.
TFF kwa sasa iko katika mpango wa kuuza tiketi za uwanjani
kwa njia ya ki-eletroniki (umeme) ikiwa ni sehemu ya jitihada ya kupunguza adha
kwa wapenzi wa soka na kudhibiti wizi na ulanguzi wa tiketi.
Wambura amesema jitihada zinafanyika kumaliza deni hilo, ila
TFF italifuatilia kwa umakini na kuchunguza mwenendo mzima uliosababisha kuwepo
deni hilo.
No comments:
Post a Comment