Alikiba anataka watu wafahamu kuwa hana na tatizo na Diamond
Platnumz na amewataka watu waache kuwakosanisha.
AliKiba amewataka
watu kuachana na tabia ya kuwagombanisha Diamond ili wafanye muziki mzuri.“Kila
mtu anaandika anachotaka juu ya mimi na Diamond, mpaka wengine wanatumia
akaunti fake za Facebook kutukosanisha, ndio maana nikasema kuna wengine
wanafanya for fun na wengine wanafanya ili kutukosanisha wengine wanafanya
lakini hawajui wanachofanya,” amesema Alikiba.
“Mimi najaribu kuwaomba wadau mbalimbali waache hiyo tabia
ya kutukosanisha kwa sababu mimi sina ugomvi na Diamond na wala sina mambo
hayo. Ninachowataka waendelee kusupport kazi zetu ili mambo yaende vizuri kwa
sababu sisi ndo wasanii wao tunaoiwakilisha Tanzania. Wanapotupa moyo wao sisi
tunazidi kukaza buti ili tufike mbali zaidi. Watu wanaotengeneza ugomvi wangu
na Diamond waache cha zaidi wafanye kusupport muziki na watuambie ni mapungufu
gani ambayo yamepungua ili tujirekebishe,”S
ameongeza.
Katika hatua nyingine, Alikiba amezungumzia mapokezi ya
wimbo Mwana na Kimasomaso pamoja na ujio wa video zake.
“Kwanza watu wamenipokea vizuri sana kama nilivyokuwa
nikitarajia, imeonyesha ni jinsi gani yale malalamiko ya maana walikuwa
wakilalamika kwamba nimekumiss na nilivyotoa nyimbo watu wanasikiliza na
kuinjoy na nyimbo zenyewe
zimekuja wakati mzuri na zenye maadili mazuri ya
kuelimisha na kuchezeka na ya kufurahisha. Maandalizi ya video yapo tayari na
booking ipo tayari vilevile, maandalizi nimeandaa hata kabla
sijatoa nyimbo, video itafanyika nje na moja ni hapa siwezi sema ni nchi gani
bado ni mapema nitasema baadae nikishaitoa, kwasababu nimetoa track mbili moja
itafanyika hapa na nyingine itafanyika nje.”
No comments:
Post a Comment