skip to main |
skip to sidebar
BALOTELLI RASMI LIVERPOOL
Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli, 24, amekamilisha uhamisho wake
kutoka AC Milan kwenda Liverpool kwa pauni milioni 16. Mchezaji huyo wa
zamani wa Manchester City, amekubali mkataba wa muda mrefu, ingawa
hatoweza kucheza dhidi ya timu yake ya zamani Jumatatu usiku. Balotelli
aliondoka City miezi 17 iliyopita baada ya kupachika mabao 30 katika
misimu mitatu.
"Uhamisho huu
unawakilisha misingi ya klabu na nadhani tumefanya biashara nzuri tu
hapa," amesema bosi wa Liverpool, Brendan Rodgers. Balotelli, ambaye
atavaa jezi namba 45, amesema alifanya makosa kuondoka England mwaka
jana. "Nimefurahi kurejea tena, kwa sababu nilifanya makosa kuondoka
England," amesema na kuongeza "Nilitaka kwenda Italy, lakini nikagundua
ni makosa."
No comments:
Post a Comment