Baadhi ya wananchi wakishuhudia jinsi miili hiyo
inavyoteketea.
Vijana wawili wakazi wa Jiji la Dar es Salaam
ambao hawakufahamika majina yao, wanaodaiwa kuwa ni vibaka alfajiri ya leo wameuawa kwa kuchomwa moto na
wananchi wenye hasira kali baada ya kumpora pochi dada mmoja mkazi wa Tabata
Liwiti. Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema baada
ya vibaka hao kumpora pochi dada huyo, walitaka kutoweka na bodaboda ndipo
wananchi walifanikiwa kumkamata aliyeipora pochi hiyo akaanguka chini wakaanza
kumpa kipigo huku mwenzake akifanikiwa kuondoka
Matairi yaliyotumika kuwachomea vibaka hao yakiungua.
Miili hiyo ikiteketea kwa moto
Kama waswahili wasemavyo za mwizi arobaini, kibaka huyo
aliyekuwa akiendesha bodaboda kwa kasi, hakufika mbali pikipiki yake ikapata
pancha naye akakamatwa na kuanza kupewa kichapo kisha walikusanywa pamoja
wakavishwa matairi na kuchomwa moto.
Baada ya kuteketea kwa moto, polisi walifika eneo la tukio
wakachukua mabaki ya miili ya vibaka hao na kuipeleka tatika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili.
No comments:
Post a Comment