Kiungo wa Real Madrid Sami Khedira hatoondoka Bernabeu msimu
huu, kwa mujibu wa kocha Carlo Ancelotti.
Khedira, 27, alihusishwa na kuhamia Arsenal na Bayern
Munich, baada ya Ancelotti kusema alikataa kusaini mkataba mpya.
"Suala la Khedira limetatuliwa. Atabakia hapa na
tumefurahishwa na hali hiyo," amesema Ancelotti.
Ancelotti pia amesema winga Angel Di Maria, 26, amewaaga
wachezaji wenzake akielekea kuhamia Manchester United.
Mabingwa hao wa Ulaya tayari wamemsajili James Rodriguez na
Toni Kroos.
Real Madrid wanacheza mechi yao ya kwanza Jumatatu dhidi ya
Cordoba iliyopanda daraja msimu huu.
No comments:
Post a Comment