Wapiganaji wa Islamic State wakidhibiti bwawa kubwa zaidi
nchini Iraq
Ndege za kijeshi kutoka Marekani zimetekeleza mashambulizi
tisa ya angani dhidi ya wanamgambo wa Islamic State kazkazini mwa Iraq ili
kuvisaidia vikosi vya Iraq kuliteka bwawa moja muhimu karibu na mji wa Mosul.
Bwawa hilo ndio kubwa nchini humo na lilitekwa na islamic
state mapema mwezi huu.
Makamanda wa Marekani wamesema kuwa mashambulizi hayo
yalioanza ijumaa usiku yaliharibu zaidi ya magari 14 ya kivita yanayomilikiwa
na Islamic State.
Duru mjini Mosul zimearifu kuwa takriban wapiganaji kumi na
moja wanadaiwa kuuawa katika shambulizi hilo.
Jenerali mmoja wa vikosi vya Kikurdi kazkazini mwa Iraq
amesema kuwa vikosi hivyo vimeanzisha mashambulizi ya kuliteka bwawa hilo
No comments:
Post a Comment