Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, August 28, 2014

PRODYUZA SUGE KNIGHT ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI,BAADA YA KUPIGWA RISASI




Prodyuza Suge Knight wakati akiwasili katika klabu ya usiku ya 1Oak ambapo baadaye alishambuliwa kwa kupigwa risasi sita.

 PRODYUZA Suge Knight ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Cedars-Sinai, Los Angeles nchini Marekani alipokuwa amelazwa baada ya kujeruhiwa kwa risasi katika klabu ya usiku ya 1Oak kwenye pati ya utangulizi wa utoaji Tuzo za VMA Jumamosi usiku.



Mmoja wa majeruhi katika shambulio hilo akipatiwa huduma ya kwanza.

 Suge aliruhusiwa jana na ataendelea na matibabu madogomadogo akiwa nyumbani kwake. 




Mbali na kujeruhiwa, Suge anadaiwa kutotoa ushirikiano kwa polisi kuhusu tukio hilo lililotokea katika pati hiyo iliyokuwa ikiongozwa na mwanamuziki Cris Brown anayedaiwa kuwa ndiye alikuwa mlengwa mkuu wa shambulio hilo.



 Mwanamitindo Megan Hawkins akiwa hospitali ya Cedars-Sinai baada ya kujeruhiwa kwenye shambulio hilo.

 Suge alipigwa risasi sita, nne tumboni, moja kifuani na nyingine mkononi ambapo watu wengine wawili akiwemo mwanamitindo Megan Hawkins nao walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Cedars-Sinai kwa matibabu.

No comments:

Post a Comment