Siku hizi ni kitu cha kawaida kuona vitu vya ajabu vikitumwa tokea akaunti ya mtu unayemuamini sana na haukutegemea kama mtu kama yeye angeweza kutuma (post) vitu kama hivyo, na ikakufanya hata utake kujitoa (Unlike / Unfriend) toka kwenye urafiki
au ufuatiliaji kwake. Je unadhani ni kweli kila kitu kinachotumwa kwenye Facebook hutumwa na na muhusika? Jibu ni hapana. Mara nyingi ni wavamizi walioingia kwenye akaunti ya muhusika na kuitumia kadri wawezavyo ama kwakuwa umeruhusu vipachiko (apps) zitume kwa niaba yako.
au ufuatiliaji kwake. Je unadhani ni kweli kila kitu kinachotumwa kwenye Facebook hutumwa na na muhusika? Jibu ni hapana. Mara nyingi ni wavamizi walioingia kwenye akaunti ya muhusika na kuitumia kadri wawezavyo ama kwakuwa umeruhusu vipachiko (apps) zitume kwa niaba yako.
Siku hizi, uvamizi wa akaunti kwenye Facebook umekuwa mkubwa, na asilimia kubwa ya uvamizi huu hutokana na ama wahusika kutofahamu athari wa wanachokichagua ama kutokujua jinsi ya kujilinda. Kama ilivyo ada, Dudumizi itakuelezea namna ya kujilinda na uvamizi huo kwenye Facebook.
Aina za uvamizi:
Kwenye facebook, kuna aina nyingi za uvamizi, lakini zilizo kubwa ni nne.
1) Mtu anayekujua kutumia akaunti yako (ana username na password yako)
2) Mtu asiyekujua kuotea (dictionary attack) namba za siri za akaunti yako (hii ni mra chache sana).
3) Kujiunga kwenye vipachiko (Apps) vinazonyonya taarifa zako ikiwemo password (Wengi ni wahanga hapa)
4. Kutumia computer ya mtu mwingine / asiye muaminifu
Kila aina ya uvamizi ina njia yake ya kujikinga, leo tutaangalia njia moja baada ya nyingine ambazo zitakuwezesha kujikinga na uvamizi huu.
i) Kutojiunga / Kuondoa vipachiko (apps) visivyo salama.
Kupambana na uvamizi wa nne, hakikisha haubonyezi tovuti (links) au kujiunga na vipachiko (apps) visizoeleweka, kwenye Facebook kuna apps nyingi sana, na kila moja huwa na machaguo yake. Jinsi uwingi wa apps unavyoongezeka ndivyo unavyojiweka kwenye hatari zaidi ya kutumiwa kwa taarifa zako.
Unapojiunga na Apps, huwa wanakuuliza je unaruhusu taarifa zako kama A,B,C zitumike? Na unaruhusu Apps kutuma kwa niaaba yako? wengi huchagua ndiyo. Na baada ya hapo ile app huanza kutuma vitu vya ajabu. Ili kujua ni apps gani zinatuma kwenye akaunti yako, nenda kwenye kikufuli halafu chagua See More Settings kama inavyoonekana chini.
Ukiwa kwenye more setting, shuka chini kabisa (upande wa kushoto) halafu bonyeza Apps
Hapa utaweza kuona Apps zinazotuma kwenye kurasa yako na nani anaweza kuona kinachotumwa na hiyo App. Bonyeza Edit iliyopo kulia kabisa kwa kila App unayotaka kuiondoa au kubadilisha, utaona machaguo yote yakiwemo taarifa zinazochukuliwa / hitajika na hiyo App. Kama hauitaki, basi bonyeza Remove Apps
ii) Hakikisha unabadilisha machaguo ya usalama.
Facebook inayo machaguo thabiti ya usalama ambayo kama utayafuata kwa umakini, kwa kiwango kikubwa utakuwa umejikinga na uvamizi mwingi unaotokana kwenye facebook, uvamizi huo ni kama namba 1,2 na 3 tuliozungumzia juu. Tuangalie ni jinsi gani utaweza kuchunga machaguo hayo.
Kama ilivyo kwenye hatua ya, nenda kwenye kikufuri, halafu See more settings, baada ya hapo bofa security.
Kwa kila chaguo, lima maana yake. Tuangalie moja baada ya lingine.
1. Taarifa za uingizaji (Login Notification)
Kwa kuchagua sehemu hii, utapokea ujumbe kwa njia ya Simu au Email pindi kama kuna mtu ameingia kwenye akaunti yako ya Facebook kwa kutumia kifaa ambacho sicho ulichotumia kuingilia kwenye facebook mara ya mwisho.
2. Login Approval
Hii ni sehemu muhimu sana ambayo unatakiwa uifanyie kazi, kwa kutumia sehemu hii, utaweza kuweka namba ya simu, hivyo, kila unapotaka kuingia kwenye Facebook, utatumiwa namba ya siri (code) ambayo utaingiza ndiyo uweze kuingia.
Kama umepoteza simu u upo mbali na simu yako na unataka kutumia kompyuta kuingia kwenye facebook, usiwe na wasi, unatakiwa kutengeneza (generate) namba za siri na kuziprint ambazo utatumia wakati wa dharura.
3. Marafiki unaowaamini (Trusted Contacts)
Waswahili husema,"Wasiwasi ndiyo dawa". Je unahofia ipo siku akaunti yako itaingiliwa na hacker kubadilisha hata password na kukufanya ushindwe kuirudisha? Kwa kutumia marafiki unaowaamini unaweza kuirudisha facebook yako. Kwenye kundi hili, unashauliwa kuweka ndugu au mke/mume (siyo wachumba). Kumbuka, watu walio kwenye kundi hili hawatoweza kuona kilichomo kwenye akaunti yako, bali tu hutumiwa pindi unapotaka kuirudisha akaunti yako iliyovamiwa na kukufanya ushiindwe kuirudisha.
4. Vifaa unavyoviamini (Trusted browsers)
Je umepoteza simu ambayo ulikuwa unaitumia kuingilia kwenye facebook na kuna mtu anaingia kwenye akaunti yako? kwa kutumia chaguo hili, utaweza kuona vifaa vyote ulivyoviamini / vilivyofanikiwa kuingia na wewe kuridhia. Hivyo unaweza kuondoa vifaa usivyotaka.
Kumbuka, kama ipo siku ulitumia kompyuta ya mtu kuingia kwenye facebook na ukaulizwa je unaamini kifaa hiki ukasema ndiyo, basi hapa ndipo sehemu ya kuviondoa.
5. Wapi uliingilia (Where You're Logged In)
Hapa utaweza kuchagua / kuona mahali (locations) ambazo ulikuwepo ulipoingia facebook. Kama haufahamu mahali hiyo, basi bonyeza End Activity na hata kama kuna mtu yupo online ataondolewa.
Hadi hapo utakuwa umeongeza usalama wa akaunti yako ya facebook, kumbuka kinga ni bora kuliko tiba na siyo kila king'aracho ni dhahabu. Kuna wavamizi wengi hutumia lugha tamu kabisa ili kuweza kupata akaunti yako.
Je unataka kujifunza zaidi juu ya mambo mbalimbali ya IT na Kekinolojia? Tembelea Blog yetu http://dudumizi.com/ resources/blog.html au jiunge kwenye facebook yetu https://www.facebook.com/ dudumizi
No comments:
Post a Comment