Belle 9 bado yupo nchini Ujerumani alikoenda kwa mapumziko
mafupi. Akiwa jijini Berlin nchini humo, hitmaker huyo wa ‘Masogange’ alitua
kwenye makao makuu ya miongoni mwa label kubwa dunia, Universal Music Group
tawi la Ujerumani.
UMG ni labal kubwa yenye label zingine ndogo ndani yake
ambazo ni pamoja na Interscope Records, Geffen Records na A&M Records na
zingine.
Belle ameiambia Bongo5 kuwa alienda kwenye ofisi hizo
kuonana na producer ambaye anafanya kazi hapo. “Nataka nifanye naye ngoma,”
amesema. “Pia jamaa ana connection ya jinsi ya kupeleka ngoma hapo.”
No comments:
Post a Comment