Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, August 22, 2014

TETESI ZA SOKA ULAYA


Juventus na Roma wanataka kumsajili beki wa kati wa Manchester City Matija Nastasic, 21, huku Newcastle na West Ham wakimtaka beki wa kulia wa Man City Micah Richards, 26, (Manchester Evening News), Manchester United wanaongoza mbio za kumsajili winga wa Real Madrid Angel Di Maria, 26 baada ya mabingwa wa Ufaransa PSG kuamua kujitoa (Daily Star), lakini Di Maria huenda asiende United kwa sababu Louis van Gaal hataki kukwaza ukuaji wa 


Adnan Januzaj, 19, (Daily Express), Tottenham wanajiandaa kutoa pauni milioni 11 kumchukua mshambuliaji wa QPR Loic Remy, 27, (Daily Star), Arsenal wanafikiria kupanda dau kumchukua beki wa West Ham Winston Reid, 26, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao (Daily Star), Hull City wameongeza dau kumchukua mshambuliaji wa Blackburn Jordan Rhodes, 24 (Daily Mail), kiungo wa Manchester United Anderson, 26, huenda akahamia Sporting Lisbon kwa pauni milioni 5.5 (Daily Express), boss wa Southampton Ronald Koeman amesema kiungo wake Morgan Schneiderlin, 24 hauzwi kwa bei yoyote (London Evening Standard), beki wa QPR Rio Ferdinand, 35, anataka kuwa meneja wa England akistaafu kucheza (Daily Mail), Newcastle United wana uhakika nahodha wao msaidizi Cheick Tiote, 28 hatoondoka licha ya timu nyingi kumnyatia (Sunderland Echo), boss wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Jack Wilshere, 22, anatolewa kafara kwa England kushindwa kufanya vizuri katika Kombe la Dunia (Sun), wakati huohuo Aaron Ramsey, 23, ana uhakika Arsenal wataweza kupambana "kwa misuli" na Manchester City na Chelsea msimu huu (Sky Sports), Barcelona wamefanya jaribio la kushangaza la kumtaka Angel Di Maria kutoka Real Madrid. Real walifikiria dau la pauni milioni 48 lakini mazungumzo ya awali yalivunjika baada ya Los Bloncos kutotaka kuwauzia mahasimu wao (Sport), Napoli wanamtazama Fabio Borini wa Liverpool, ambaye kuwasili kwa Mario Balotelli huenda kukasaidia kufanikisha uhamisho wake (Tuttosport), dau la Manchester United kumtaka Nicolas Gaitan limekataliwa na Benfica (Record), Arsenal wanafikiria kumchukua William Carvalho kutoka Sporting, huku Sami Khedira anaweza kwenda Emirates iwapo atashusha madai ya mshahara mkubwa (Daily Telegraph), AC Milan wanajiandaa kumtaka mshambuliaji wa Tottenham Roberto Soldado kuziba pengo la Mario Balotelli anayeelekea Liverpool. Spurs watamruhusu Soldado kuondoka na nafasi yake kuzibwa na Loic Remy kutoka QPR (Daily Mail), Manchester United na Zenit St Petersburg wapo tayari kupambana kumwania kiungo wa Inter Milan Fredy Guarin (Corriere dello Sport), Barcelona wanatumaini kukamilisha usajili wa Marco Reus kutoka Bayern Munich.

Maafisa wa Bayern wana wasiwasi kuwa huenda mchezaji huyo tayari amekubali kujiunga na Catalans ambao huenda wakafungiwa kusajili (Mundo Deportivo). Zimesalia siku 10 kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!!

No comments:

Post a Comment