Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, August 23, 2014

TETESI ZA SOKA ULAYA



Mshambuliaji wa England Danny Welbeck, 23, ameambiwa anaweza kuondoka Manchester United, wakati Louis van Gaal akiendelea kukisuka kikosi chake. Tottenham wameonesha nia ya kumtaka Welbeck (Times), mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Eto'o, 33, amefanyiwa vipimo vya afya Liverpool na atasaini mkataba wa mwaka mmoja Anfield (Daily Mirror), meneja wa Sunderland Gus Poyet hajakata tamaa kumsajili mshambuliaji wa 


Liverpool Fabio Borini, 23, na anataka kuchukua wachezaji wengine wawili kwa mkopo (Daily Express), Barcelona walitoa dau la pauni milioni 48 kumtaka winga wa Real Madrid Angel Di Maria, 26, lakini ombi hilo lilikataliwa mara moja na rais wa Real Florentino Perez (sport.es), kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Pogba, 21, amefuta matumaini yoyote ya kurejea Old Trafford baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitano Juventus (Daily Star), Liverpool wamemuambia Mario Balotelli kuwa atapoteza pauni milioni 2 kwa mwaka iwapo ataonesha utovu wa nidhamu, baada ya pia kukubali kupunguza mshahara wake kutoka AC Milan (Sun), AC Milan wanatazama kati ya wachezaji sita kuziba pengo la Balotelli, akiwemo Javier Hernandez, 26, wa Man U, Roberto Soldado, 29, wa Spurs na Fernando Torres, 30, wa Chelsea (Gazetta dello Sport), Arsenal wanakaribia kumsajili beki wa Olympiakos Kostas Manolas, 23, kuziba pengo la Thomas Vermaelen aliyekwenda Barcelona (Goal), kipa wa Stoke City Asmir Begovic, 27, hatoondoka kabla ya dirisha la usajili kufungwa licha ya Liverpool, Manchester City, Arsenal na Real Madrid kuonesha dalili za kumtaka (Daily Mirror), AC Milan wanamtaka kiungo wa Chelsea Marco van Ginkel kwa mkopo (Inside Futbol), boss wa Sunderland Gus Poyet anamtaka Danny Welbeck wa Man U kwa mkopo (Sunderland Echo), Fredy Guarin anayesakwa na Man U anajiandaa kujiunga na Zenit St Petersburg baada ya Andre Villas Boaz kumshawishi mchezaji huyo kutoka Colombia kuhamia Urusi, ingawa lazima kwanza wafuzu kucheza Champions League (Gazetta dello Sport), Napoli wanafikiria kumchukua Marouanne Fellaini licha ya kumsajili Jonathan de Guzman (Corriere dello Sports), mshambuliaji wa Arsenal Lukas Podolski anajiandaa kurejea Ujerumani na kujiunga na Wolfsburg. Galatasaray na Besitkas wanamtaka mchezaji huyo, lakini anaonekana kwenda Bundesliga (Metro). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Zimesalia siku tisa kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Cheers!!

No comments:

Post a Comment