Arsenal wapo tayari kutoa dau la pauni milioni 50 kumtaka
Edinson Cavani kutoka Paris St-Germain, kutokana na Olivier Giroud kuwa na
uwezekano wa kutocheza kwa muda mrefu kutokana na jeraha la mguu (Daily
Express), Arsenal pia wanamtaka Danny Welbeck, 23, kutoka Manchester United,
kuziba nafasi ya Giroud, lakini Man U wanasita kumuuza Welbeck (Daily Mail),
boss wa Arsenal vilevile anataka
kumchukua kwa mkopo Radamel Falcao, 28, kutoka
Monaco, na pia Loic Remy, 27, ambaye anapatikana kwa pauni milioni 8.5 kutoka
QPR (the Guardian), boss wa Manchester United Louis van Gaal anafikiria kutaka
kumsajili kiungo wa Liverpool Joe Allen, 24, kwa kutoa pauni milioni 20, (Daily
Star), United wanafanya mazungumzo ya kumsajili Daley Blind, 24, huku kipa wa
zamani wa Man U, Edwin van der Sar akiwa Manchester kukamilisha uhamisho wa
beki huyo wa Ajax (Daily Star), Manchester United pia wanafikiria kumtoa Shinji
Kagawa, 25, au Javier Hernandez, 26, kama chambo katika mkataba wa kumchukua
kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, (Independent), Real Madrid watatumia kiasi
kikubwa cha fedha za mauzo ya Angel Di Maria, kumnunua mshambuliaji wa Monaco,
Radamel Falcao (Le Sport), AC Milan wamethibitisha kuwa wanataka kuwasajili
Fernando Torres, 30, na kiungo Marco van Ginkel, 21 kutoka Chelsea (Daily
Express), AC Milan wamechoka kumsubiri Torres kuamua anataka nini na wamempa
makataa, huku wakijiandaa kuanza kumfuatilia Roberto Soldado, 29, kutoka
Tottenham au Fabio Borini, 23, wa Liverpool (Inside Futbol), Tottenham
wanajiandaa kukamilisha usajili wa beki wa Sevilla Federico Fazio, 27, baada ya
kulipa pauni milioni 8 za kipengele cha ununuzi (Daily Telegraph), Spurs pia
wanafikiria kumfuatilia kiungo kutoka Cameroon Alexandre Song, 26, ambaye
ameambiwa anaweza kuondoka Barcelona bure (the Times), boss wa QPR Harry
Redknapp yuko tayari kupanda dau kwa kiungo wa West Ham Mohammed Diame, 27,
(Daily Mirror), Alvaro Arbeloa anataka kuondoka Real Madrid kabla ya dirisha la
usajili halijafungwa (El Chiringuito), Manchester United wanajiandaa kutoa dau
jipya la pauni milioni 33.4 kwa Juventus kumtaka Arturo Vidal (Gazzetta dello
Sport), Real Madrid watapambana na Barcelona na Atletico Madrid kutaka
kumsajili Marco Reus kutoka Borussia Dortmund (AS), Hatem Ben Arfa anataka kubakia
Newcastle licha ya meneja Alan Pardew kutompanga (Newcastle Evening Chronicle),
Arsene Wenger anataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Birmingham City,
Nikola Zigic ambaye ni mchezaji huru (www.zurnal.rs). Share tetesi hizi na
wapenda soka wote. Zimesalia siku tano kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.Na Salim Kikeke
No comments:
Post a Comment