Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, September 18, 2014

IDADI YA WALIOKUFA KATIKA KANISA LA NABII TB JOSHUA INATISHA, WAMO RAIA 67 WA AFRIKA KUSINI

Maiti nyingi bado zimefukiwa katika kifusi hiki na jitihada za uokoaji zinaendelea.
Idadi ya watu waliokufa kwenye Kanisa la Synagogue of All Nations (SCOAN) la Nabii TB Joshua nchini Nigeria inatisha baada ya Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, kusema raia 67 wa nchi nao wamepoteza maisha.
 Taarifa ya Rais Zuma iliyotolewa jana Jumanne inasema 


kwamba vifo vya raia hao wa Afrika Kusini vimethibitishwa rasmi na ubalozi wa Afrika Kusini nchini Nigeria.
Mamia ya watu waliojeruhiwa vibaya baada ya kanisa hilo kuporomoka Ijumaa iliyopita.

“Huu ni wakati mgumu sana kwa Afrika Kusini. Katika historia ya karibuni ya nchi hii hatujawahi kuwa na idadi kubwa kama hii ya vifo vya mara moja nje ya nchi yetu," alisema Rais Zuma.
“Tunazihuzunikia familia, marafiki na jamaa za waliopoteza maisha.
“Taifa zima linaungana nao katika majonzi ya mama, baba. mabinti na vijana waliopoteza wapendwa wao. Sote tupo katika maombolezo,” alisema.
Jumanne jioni, Clayson Monyela, msemaji wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa aliandika kwenye akaunti yake ya tweeter kwamba serikali ilikuwa inahangaika kupata taarifa za janga hilo.
Zuma alisema alikuwa ameziagiza idara mbalimbali za serikali kuhakikisha kwamba ndugu wa marehemu hao wanapelekwa Nigeria kutambua miili ya ndugu zao na kwamba serikali imeagiza miili hiyo irejeshwe haraka nyumbani Afrika Kusini.

Taarifa hizo zimekuja kwa mshtuko kwamba yawezekana waliokufa ni zaidi ya 100 kwani jengo hilo la kanisa, ambalo lina nyumba ya kulala wageni, lilikuwa na watu wengi kutoka mataifa mbalimbali wakati linaporomoka.

No comments:

Post a Comment