Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, September 10, 2014

Makubaliano ya JK na ukawa ni haya hapa

picha na maktaba




.katiba ya zamani kufanyiwa marekebisho

.Ni kuruhusu tume huru na mgombea binafsi

.Ni makubaliano ya viongozi wa vyama vya siasa

Na Lukwangule Blog

KATIBA inayotumika sasa ya mwaka 1977 itafanyiwa marekebisho muhimu kupisha uchaguzi mkuu ujao, na Rais ajaye ataamua hatima ya katiba mpya ya Tanzania.


Hayo yametamkwa leo na Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo akizungumza na waandishi wa habari .

Kwa matamko ya Cheyo mchakato wa kuandika katiba umesitishwa.

Cheyo amesema kwamba hayo ni maamuzi yaliyofikiwa na viongozi wa vyama vya siasa vyenye wabunge na Rais Jakaya Kikwete.

Mambo ambayo vyama vya siasa wamekubaliana ni kuwa na tume huru ya uchaguzi na kusimamia uchaguzi wa mwaka 2015, mshindi wa uchaguzi wa Rais ashinde kwa zaidi ya asilimia, matokeo ya uchaguzi wa rais yaweze kupingwa mahakamani na kuruhusu mgombea binafsi katika uchaguzi.

Pia vyama vingine vya siasa ambavyo vinapenda kupendekeza mambo mengine ya kurekebisha katika katiba ya mwaka 1977 vinaombwa kufanya hivyo mapema kwa kuwa muda uliopo wa kufanya mabadiliko ni mdogo.

“Muda tulio nao ni kwa mabadiliko yanayopendekezwa kujadiliwa  katika Bunge la Novemba na wakichelewa Bunge la Februari 2015,” alisema Cheyo.

Kwa makubaliano hayo, kazi inayofanywa na Bunge maalum la katiba (BMK)  ya kuandika katiba mpya itakoma Oktoba 4 mwaka huu, siku ambayo  Bunge hilo litakuwa halijakamilisha uandikaji wa katiba ambao unafanywa na kamati ya uandishi iliyo chini ya Andrew Chenge.

Uamuzi huo unakidhi baadhi ya madai ya kundi linalojiita umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ambao ni wajumbe waliokuwa ndani ya Bunge maalum la katiba lakini walijiondoa kwa kutoridhishwa na mwenendo wa bunge hilo.

Miongoni mwa madai yao waliyokuwa wanayataka ya kusitisha Bunge hilo hayakufanikiwa kwani litaenda hadi mwisho.

No comments:

Post a Comment