INAUMA sana! Wakati Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro likimshikilia
mkazi wa wilayani Mvomero, Johnson Damian Mkude kwa msala wa kumchinja mdogo
wake na kupeleka kichwa kwa mganga wa kienyeji ili awe bilionea, jeshi hilo
linamshikilia mfanyabiashara mwingine maarufu mkoani hapa aitwaye Lyimo kwa
tuhuma za kumcharanga mapanga Damas Valeniani (36) ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino).
Dada wa Damas Valeniani.
“Kulipokucha ndipo tukaenda kuripoti polisi na kupewa jalada
la kesi namba MOR/RB/5122/2014-SHAMBULIZI.
“Polisi walifika nyumbani na kumkamata mtuhumiwa na
kumfikisha kwenye mkono wa sheria na mimi nikapewa PF-3 kwa ajili ya matibabu
kwenye Hospitali ya Mkoa wa Morogoro,” alisema Damas kwa maumivu makali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, SAC Leonard Paul
akifafanua jambo.
Akihojiwa na mwandishi wetu juu ya tukio hilo, mwenyekiti wa
mtaa huo, Ally Malekela alikiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba Lyimo
alipewa saa 24 za kuhama kwenye mtaa huo.
Wananchi mbalimbali waliozungumza na Ijumaa Wikienda,
walisema Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, SAC Leonard Paul, anatakiwa
kufanya kazi ya ziada ili kukabiliana na matukio kama hayo.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Mkoa wa
Morogoro, David Mganga alisema: “Natoa wito kwa jamii ielewe kuwa kiungo cha
albino hakiwezi kumpa mtu utajiri au mafanikio, waache kututesa sisi maalbino.”
No comments:
Post a Comment