Aina mpya ya Dinosaria imetambuliwa kufuatia kupatikana kwa
mifupa nchini Tanzania.
Mabaki hayo ya Dinosaria yaliyopewa jina la - 'Rukwatitan
Bisepultus' - yalipatikana katika korongo moja kwenye eneo la Rukwa, kusini
magharibi mwa nchi hiyo.
Inadhaniwa mnyama huyo aliyekuwa akiishi kwa
kula majani,
aliishi karibu miaka mia moja iliyopita, na alikuwa na uzito sawa na tembo
kadhaa na alikuwa na miguu ya mbele yenye urefu wa mita mbili.
Mnyama huyo ni aina ya Titanosaurus -- ambao ni wakubwa, na
wanaokula nyasi.
Mabaki ya wanyama aina hiyo mpaka sasa yamepatikana katika
maeneo ya Amerika ya Kusini, bara ambalo lilijitenga kutoka Afrika katika
kipindi cha Cretaceous, (kipindi ambacho miamba ya chokaa iliumbika) takriban
miaka milioni mia moja na arobaini iliyopita.
No comments:
Post a Comment