Denti wa darasa la tano anayetambulika kwa jina moja la Irene
(11) aliyenaswa akiwatapeli raia.
Nyuma ya tukio la
denti wa darasa la tano kwenye shule moja ya msingi iliyopo Mbezi-Shamba, Dar,
aliyejitambulisha kwa jina moja la Irene (11) la kunaswa akifanya utapeli kwa
kuwaibia raia, mazito yameibuka.Katika tukio hilo lililojiri hivi karibuni
maeneo ya Posta Mpya, Dar, denti huyo alikuwa akisimama nyakati za asubuhi
akivalia sare za shule huku akiombaomba kwa madai kuwa hana nauli ya kuvukia
katika kivuko cha
Kigamboni kwenda shule anayosoma. Kwa mujibu wa mmoja wa
mashuhuda, mtoto huyo alikuwa akisimama mbele
ya Kituo cha Daladala cha Posta mpya akijifanya ombaomba kwa madai
kwamba hana nauli.Ilisemekana kwamba
siku nyingine mtoto huyo alikuwa akionekana akiuza simu kwa bei chee na
alipohojiwa alikokuwa akizitoa alidai ameziokota.
Mwandishi Gabriel
Ng'osha (kushoto) akipata undani wa habari katika tukio hilo.
Dereva mmoja, Juma
Hamis anayeegesha gari lake eneo hilo (Posta Mpya) alisema kuwa tabia ya mtoto
huyo ilikuwa ni ya muda mrefu kwani alianzia Kariakoo, Dar akitapeli na kuiba
madukani ambapo watu walimstukia hivyo akaamua kuhamia Posta. “Mara kadhaa
amenusurika kupigwa akidaiwa kuchomoa simu za watu kwenye mikoba ndani ya
daladala.“Kukamatwa kwa Irene, watu wa maofisini na kwenye daladala wameshukuru
kwani anafahamika na ni tishio kwa utapeli na ndiyo waliomchoma kwa polisi
akadakwa baada ya kukutwa akijidai ni ombaomba,” alisema dereva huyo.
Afisa wa Polisi kutoka 'Central Police' Posta akifafanua
jambo kuhusiana na mkasa huo.
Jader Sapi,
anayefanya kazi katika ofisi moja zilizo ndani ya jengo la IPS, alisema mtoto
huyo aliwahi kuingia ofisini kwao na alipotoka, wafanyakazi wawili walilalamika
kupotea kwa simu zao, kitu kilichowafanya wajue ni yeye. Mama mmoja
aliyeshuhudia Irene akichukuliwa na askari, alisema ameshawahi kumpa fedha mara
kadhaa denti huyo, akiamini alivyomweleza kuwa hakuna na wazazi na hivyo hana
nauli ya kumpeleka shuleni.
Akizungumza na gazeti hili akiwa mikononi mwa polisi kwenye
Kituo Kikuu, Irene alisema ni mwanafunzi wa shule moja ya msingi (jina kapuni)
iliyopo Mbezi-Shamba na siyo kama alivyokuwa akidanganya kuwa anasoma
Kigamboni, Dar.
Wananchi wakishuhudia laivu tukio hilo lililotokea maeneo ya
Posta mpya, Dar es Salaam.
Pia alikiri kwamba
amekuwa akidanganya kuwa hana wazazi wakati ukweli ni kwamba wazazi wake
wapo.“Ni shetani tu aliniingia nikawadanganya raia,’’ alisema Irene.
Baada ya kushuhudia tukio hilo, wanahabari wetu walimsaka
mkuu wa shule anayosoma mtoto huyo, Yusuph Zenny ambaye alikiri kumfahamu Irene
na kudai kuwa tayari taarifa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi, Dar zilimfikia.
Alitobosa siri kuwa ameshapata malalamiko mara kadhaa
kuhusiana na binti huyo na kwamba amekuwa akifanya uchunguzi ili kupata ukweli.
Hata hivyo, alisema anawasiliana na wazazi ili kulifuatilia
sakata hilo hivyo kuwaomba wanahabari wetu wampe muda atatoa majibu au hatua
itakayochukuliwahuku Irene akiwa bado mikononi mwa polisi kwenye dawati la
jinsia.NA GPL
No comments:
Post a Comment