Upasuaji huo umesemekana kufanywa kwa uangalifu mkubwa
kutokana na hofu yatisho kwa maisha ya Samaki huyo.
Samaki huyo kwa jina George, ambaye mmiliki wake anaishi
Melbourne, alidunguwa sindano ya kuondoa fahamu iliyogharimu dola 200.
Daktari Tristan Rich, aliyefanya upasuaji huo, aliambia
kituo cha redio cha 3AW mjini Melbourne kuwa Samaki huyo kwa sasa amepata
fahamu na tayari ameanza kucheza na kuogelea majini.
Wataalamu wa matibabu ya wanyama, wanasema kuwa Samaki huyo mwenye umri wa miaka 10, anatarajiwa kuiishi kwa miaka mingine 20.
"George alikuwa na uvimbe mkubwa sana kwenye ubongo wake na alikuwa anakuwa polepole sana, na hali hiyo ilikuwa inaanza kuathiri maisha yake,'' alisema daktari Rich kutoka hospitali ya matibabu kwa wanyama ya Lort Smith.
Mmiliki wa George, alikuwa ameambiwa achague kati ya Samaki huyo kufanyiwa upasuaji au adungwe sindano ya kulala.
Lakinin aliona bora kujaribu kuokoa maisha ya Samakai wake na ndipo akakubali Samaki huyo afanyiwe upasuaji.
Aliongeza kuwa Samaki huyo alisalia kuwa hai kutokana na madaktari kuweka hewa ya Oxygen kwenye maji wakati wa upasuaji.
No comments:
Post a Comment