Meneja Mawasiliano kutoka
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo
pichani) kuhusu matumizi mabaya ya mawasiliano na udanganyifu katika usajili wa
namba za simu za mkononi leo Jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………
Serikali yawatahadharisha wananchi kuhusu matumizi mabaya ya
Mawasiliano na udanganyifu katika usajili wa namba za simu za mkononi kwa kuwa
ni kosa la jinai.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) bw. Innocent Mungy amesema kumekuwa na watu
wachache wanaotumia mawasiliano pasipo kuzingatia sheria na kanuni.Kumekuwa na
matukio yanayoashiria kutumika kwa mitandao ya kijamii kuleta madharambalimbali
kwa watumiaji ikiwemo utapeli,kulipiza kisasi, ugomvi,kuwaumiza wengine kwa
mambo yasiyo na ukweli na kuvuruga kwa ujumla alisema MungyAkifafanua Mungy
amesema pamoja na maendeleo chanya katika Sekta ya Mawasiliano kumekuwa na watu
wachache wanaotumia simu,mitandao ya kijamii,redio,televisheni, na mawasiliano mengine kwa lengo la kuvuruga
amani.
Kutokana na hali hiyo Mungy amesema kuwa TCRA inawakumbusha
wananchi wote kwamba ni kosa la jinai kutumia mawasilano vibaya kama
ilivyoainishwa kwenye sheria ya
mawasiliano ya kielektroniki na Posta ( EPOCA) ya mwaka 2012.
Pia Mungy alitoa wito kwa wananchi na watumiaji wa simu za
mkononi kuunga mkono juhudi za Serikali ili wananchi wote wasajili namba za
simu kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani ,usalama na kuharakisha
maendeleo ya sekta hii na Taifa kwa ujumla.Naye Naibu Mkurugenzi Masuala ya
Huduma kwa wateja toka mamlaka hiyo Bw. Isaac Mruma amesema ni vyema wananchi
wakazingatia matumizi sahihi ya mawasiliano kwa maslahi mapana na Taifa.Sheria
ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) mwaka 2010, kifungu cha 131
imeainisha kuwa ni kosa la jinai kutumia au kuwezesha kutumika kwa namba ya simu
isiyosajiliwa na adhabu yake ni faini ya shilingi laki tano (Tsh. 500,000) au
kifungo cha miezi mitatu kwa atakayekiuka sheria hii
No comments:
Post a Comment