Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, September 9, 2014

Waziri Membe apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Mabalozi wapya wa Rwanda na Norway hapa nchin


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mpya wa Rwanda hapa nchini, Mhe. Eugen Sayore Kayihura. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ofinini kwa Mhe. Membe tarehe 08 Septemba, 2014.
Waziri Membe akizungumza na Balozi Kayihura mara baada ya kuwasilisha Nakala za hati za utambulisho. Katika mazungumzo hayo Mhe. Membe alimhakikishia ushirikiano Balozi huyo na kumwomba awe huru katika kutekeleza majukumu yake ya kazi wakati wote akiwa hapa nchini.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Norway hapa nchini, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad. Hafla hiyo ilifanyika Ofisini kwa Mhe. Waziri tarehe 08 Septemba, 2014.
Mhe. Membe akizungumza na Balozi Kaarstad mara baada ya kupokea Nakala za hati za utambulisho za Balozi huyo.
Mhe. Membe akiagana na Balozi Kaarstad.

No comments:

Post a Comment