Aslay akimwagiwa minoti na Beutiful Onyinye, Wema Sepetu
‘Madam’. Tukio hilo limetokea ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem
na kuweka historia kwa Wema kuwa staa wa kwanza ‘kumwaga’ fedha wakati wa
uzinduzi wa bendi ya Yamoto.
Awali, wakati bendi ya Yamoto ilipokuwa ikitumbuiza, ulifika wakati kiongozi wa bendi hiyo, Said Fella alitambulisha uwepo wa Wema kwa kudai amemuwakilisha bebi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivyo apande jukwaani na kusema chochote lakini mrembo huyo akasema kilichompeleka ukumbini hapo ni uzinduzi wa Yamoto Band.
“Jamani nimekuja hapa kwenye uzinduzi wa Bendi ya Yamoto na siyo kumuwakilisha Diamond, ya huku hayamuhusu kabisa sasa semeni niwaimbie wimbo gani,” alisikika Wema Sepetu na kuanza kuimba wimbo wa Niseme ambao mashabiki waliupendekeza. Aslay akifurahiya minoti aliyomwagiwa na Beutiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’.CHANZO GPL



No comments:
Post a Comment