KUMBE! Pia mume wa mtu ni sumu! Kikongwe wa miaka 70
aliyejitambulisha kwa jina la Gwerino Ganga amemtwanga risasi mbili mwanaume
aitwaye Thadei Mbungu (40) akimtuhumu kuingilia ndoa yake kwa kuvunja amri ya sita na mama watoto wake.
Thadei Mbungu enzi wa uhai wake.
Tukio hilo la ajabu lilijiri Oktoba 9, mwaka huu mkoani Iringa ambapo mashuhuda wanadai Mbugu, mbali na kukutwa na mke wa mtu siku hiyo, alimjibu mwenye mke majibu yenye kuumiza moyo mbele ya watu waliokuwa wakinywa pombe katika klabu cha pombe za kienyeji.
Ilidaiwa kuwa, awali mtuhumiwa huyo wa mauaji alikuwa akimsaka marahemu ambaye alidai amekuwa akiivuruga ndoa yake.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyefika eneo la tukio, mtoto wa kambo wa mtuhumiwa alisema chanzo cha mauaji hayo ni mke wa Mbungu kumtuhumu mama yake (mke wa mtuhumiwa) kuwa ana tabia ya kukopa fedha kwa mumewe (marehemu) hali iliyosababisha mama huyo kwenda kumwita baba yake (mtuhumiwa) na kumshitakia maneno hayo.
Mke wa mtuhumiwa.
Baada ya kufikishiwa
malalamiko hayo, mzee huyo alifika ndani
ya klabu hicho na kuanza kumuuliza
marehemu juu ya uhusiano wake na mkewe,
ndipo marehemu alipotoa lugha chafu mbele ya watu
kwa mwenye mke kuwa ni maskini,
hana uwezo wa kutunza wake zake wawili hivyo anasaidia kulea.
Kufuatia kauli hiyo, mtoto huyo wa mtuhumiwa alisema baba
yake alimtaka marehemu na mkewe kuondoka
klabuni hapo kwa vile wamependana na kwenda kuishi pamoja lakini marehemu aligoma na kuendelea
kutoa lugha yenye kuudhi.
“Baada ya hapo mimi nilitoka
kwenda kutafuta msaada wa watu
kuja kuamua ugomvi huo kwa kumtoa marehemu, lakini ghafla nilisikia mlio wa risasi, nikarudi mbio na
kukuta marehemu akitoka nje huku akivuja
damu baada ya kupigwa risasi ya bega la kushoto,” alisema mtoto huyo.
Gwerino Ganga anayetuhumiwa kwa kosa la mauaji.
“Nilitoka kwenda kutafuta msaada wa gari, sikupata, wakati
narudi baba alimuongeza risasi nyingine na kumuua kabisa,” aliongeza.Ikadaiwa
kuwa, baada ya kumuua kabisa mgoni wake, mzee huyo alitaka kumpiga
risasi mkewe lakini wananchi walifika na kumpokonya bunduki kisha kumtia nguvuni.
Mke wa mtuhumiwa huyo,
Melea Mtwanga alisema hajapata kuwa na uhusiano wa mapenzi na marehemu
ila aliuawa kwa sababu ya lugha zake chafu.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye eneo la tukio.
“Marehemu alikuwa akinidai pesa za mahindi debe kumi na
wakati akinidai, ghafla mume wangu alitokea na kumuuliza kwa nini unaongea na
mke wangu, akajibu majibu machafu ndipo
alipompiga risasi huku akiwa amekaa kwenye benchi akinywa pombe na wenzake,”
alisema mwanamke huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na mtuhumiwa anashikiliwa huku akisema
bunduki hiyo aina ya shot gun ilikuwa ikimilikiwa kihalali.
No comments:
Post a Comment