Jeshi la polisi wilayani Ludewa likiondoka eneo la tukio
majirani wakiuangaliwa mwili wa marehemu Mgimba.
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Merkion
Mgimba(Msuruisi) miaka 70 mkazi wa Ludewa Kijijini katika wilaya ya Ludewa
Mkoani Njombe ameuawa kwa kupigwa nondo kichwani usiku wa kuamkia tarehe 28
oktoba 2014 akiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana.
Akitoa
taarifa katika eneo la tukio mke wa marehemu Bi.Theodora Luoga alisema kuwa
marehemu alitoka ndani majira ya saa 5 usiku kwa lengo la kujisaidia haja ndogo
lakini ghafla alikutana na mtu nje ya nyumba yake na kuanza kupambana naye
ndipo alipozidiwa nguvu na kukimbilia ndani akipiga kelele.
Bi.Theodora
alisema baada ya kusikia kelele hizo sebuleni alilazimika kutoka chumbani ili
aende kutoa msaada kwa mume wake lakini alipofungua mlango wachumbani alikutana
na nondo iliyompata mkononi ndipo alipofanya uamuzi wa kutokea dirishani ili
aende kuomba msaada lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda kwani alishuhudia mtu
aliyevalia shati jeupe akitokomea gizani.
Alisema
baada ya muuaji huyo kukimbia alirudi kuona hali ya mumewe lakini alimkuta
tayari ameshaaga Dunia,hapo akachukua uamuzi wa kwenda kuwaeleza majirani na
kiongozi wa mtaa ili kumsaka muuaji huyo ambaye hakuweza kumfahamu zaidi ya
kushuhudia shati lake jeupe.
“Nilisikia
mumewangu akikimbia kutoka nje na baadae kelele sebuleni ndipo nilipotoka ili
kutoa msaada lakini nilipofungua mlango wa chumbani muuaji huyo alinipiga na
nondo mkononi ikanilazimu kufunga mlango na kurudi chumbani nikisikia mume
wangu akilia kwa uchungu,nikaamua kupitia dirishani ili niombe msaada kwa majirani
ndipo nilipomuona muuaji huyo akikimbia kichakani”,Alisema Bi.Theodora.
Alisema
muuaji huyo hajachukua kitu chochote zaidi ya kufanya mauaji,pia alithibitisha
kuwa hii ilikuwa ni awamu ya pili kwani kunakipindi marehemu aliwahi kupambana
na mtu nje ya nyumba yake nyakati za usiku na kumshinda mtu huyo alibeba nondo
kama ilivyokuwa leo ila hakutambulia.
Aidha
kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Njombe SACP Fulgence Ngonyani amethibitisha
kutokea tukio hilo alisema mpaka sasa bado jeshi la polisi linaendelea na
upelelezi wake ili kumbaini muujia taarifa kamili zitatolewa upelelezi ukikamilika.
NA HABARI LUDEWA BLOG.
No comments:
Post a Comment