Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki
kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani
akisherehekea bao lake.
Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti
wake wa mgongo baada ya kupiga pindu uwanjani akisherehekea bao lake la
kusawazisha kw atimu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC.
Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa
upasuaji
lakini baadaye alifariki.
Mechi hiyo ambapo alipata jerehe la mgongo, ilikuwa mechi
muhimu katika ligi ya nchi hiyo.
Taarifa kutoka kwa ligi hiyo kpitia kwa mtandao wa Facebook,
ilisema : ''imekuwa siku yenye huzuni mkubwa kwa ligi ya Mizoram na kifo cha
mchezaji wetu kimetushtua sana pamoja na wachezaji wenzake, wachezaji wa soka
na mashabiki wa Mizoram. ''
"Peter alikuwa mchezaji mzuri na milizni mzuri sana, na
pia alikuwa mchapa kazi.''
No comments:
Post a Comment