Wawili hao sasa wanaweza kutunda matunda bila tatizo lolote.
Kwa mujibu wa jarida la tiba ya sayansi, sensa zilizopo
katika mkono huo bandia hutumiwa kutuma ishara moja kwa moja katika mwili.
Wakati huohuo kundi moja la wanasayansi wa Sweden limefanya
uvumbuzi mwengine wa viungo bandia,unaoshikanisha mkono huo bandia moja kwa
moja na mfupa ili kuimarisha udhibiti.
Mmoja wa watu waliofaidika na uvumbuzi huo wa
Marekani ni
Igor Spetic aliyepoteza mkono wake wa kulia kupitia ajali miaka minne iliopita.
Aliwekewa mkono wa bandia lakini hakuweza kuhisi chochote.
Ilimbidi awe mwangalifu katika chochote kile alichokuwa
akifanya na kuweza kutumia macho yake kubaini iwapo alikuwa akitumia nguvu au
la wakati anaposhika kitu.
Lakini kundi moja la wanasayansi katika chuo kiikuu cha Case
Western Reserve liliweka sensa katika mkono huo wa bionic ambayo iliweza kutuma
ujumbe wa msisimuko wa kielektroniki katika ubongo wake.
Itikio la ubonge liliweza kutuma ujumbe katika maeneo 19 ya
mkono kutoka katika kiganja hadi katika dole gumba.
Hatua hiyo ilimwezesha bwana Spetic kujua iwapo anashikilia
kitu au la.Mtu huyo ameweza kuutumia mkono huo kwa miaka miwili na nusu.
No comments:
Post a Comment