Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, October 28, 2014

MKUTANO WA HALIMA MDEE WAINGIA DOSARI BAADA YA VIJANA WA CCM KUUVAMIA NA KUSABABISHA VURUGU



Mkutano wa mwenyekiti wa baraza la wanawake  wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Halima Mdee umeingia dosari baada ya vijana wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa chama cha mapinduzi CCM kuingia na mabango yao katika mkutano uliokuwa ukifanyika kijiji cha Kyamiorwa kata Kashalunga  wilayani Muleba na kusababisha vurugu.
Mwenyekiti wa baraza la wanawake Chadema Halima Mdee amepokelewa leo katika kijiji cha Kyamiyorwa na kufanya mkutano na wananchi katika kijiji hicho ambapo vijana wanne wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa chama cha mapinduzi CCM walipoingia katika mkutano huo huku wakiwa wameshikilia mabango yao na kusababisha vurugu katika mkutano huo, vurugu hiyo zimetulizwa na jeshi la Polisi na mpaka sasa jeshi hilo linamshikilia kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Mansud Amri ambaye ametajwa kuhusika katika kufanya vurugu hizo.




Akiongea katika mkutano huo mwenyekiti wa bara la wanawake wachama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Halima Mdee amewataka vijana kutotumiwa na wanasia wanao lenga kuvuruga amani ya nchi na badala yake watulie ili kujenga taifa lenye amani na utulivu.

Nao baadhi ya wafuasi wa chama hicho akiwemo mbunge wa viti maalumu Conchester Rwamlaza wamewataka wananchi kutoiunga mkono katiba mpya na akaongeza kuwa wananchi wanatakiwa kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kuhakikisha wanachagua viongozi bora ambao wataliongoza taifa hili kwa umakini.

No comments:

Post a Comment