Watu katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu wameanza kutumia
mtambo wa kwanza kuwahi kutumika wa kutoa pesa mjini humo.
Mtambo huo wa benki ya Salaam Somali Bank, umewekwa katika
hoteli moja na tayari umeanza
kutumika na kuwaruhusu wateja kutoa dola za
kimarekani.
Mtambo wenyewe uko karibu na hoteli ya kifahari ya Jazeera ambayo
ina ulinzi mkali sana.
Watu wengi wameshangazwa na mashine hiyo kwa kuwa hawajawahi
kuiona na hata kuitumia.
Sekta ya benki nchini Somalia, bado sio thabiti huku
wafanyabiashara wengi na familia zao wakitumia vijisanduku vya siri kuweka
akiba zao.
Banki hiyo imesema inajiandaa kuweka mitambo mingine ya pesa
mjini humo.
Wadadisi wanasema hii ni ishara kwamba mji wa Mashambulizi
ya mara kwa m ara yaliyokuwa yakifanyika mjini Mogadishu yamepungua huku
angalau hali ya utulivu ikianza kushuhudiwa.
No comments:
Post a Comment