Kufuatia taarifa zilizozagaa mjini morogoro na kuripotiwa
kwenye mitandao ya kijamii kuwa mbunge wa jimbo la morogoro kusini, Dk Lucy
Nkya na mwanaye Jonas Nkya ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa
kupitia vijana, kurushiana risasi kwenye ofisi yao binafsi ya faraja trust
fund, watu hao wawili wamekanusha madai hayo na kudai yameleta athari kubwa katika familia yao.
Awali taarifa zilizojitokeza na baadaye kurushwa kwenye
mitandao mbalimbali ya kijamii, ilikuwa ni
mama huyo aliyewahi kuwa naibu
waziri wa afya, na mwanaye ambaye ni mjumbe wa NEC akiwakilisha vijana,
kurushiana risasi kwa kugombea nyumba iliyotaka kuuzwa jijini Dar es salaam,
hali iliyofanya ITV kumtafuta kamanda wa
polisi mkoa wa morogoro Leonard Paulo ambaye kwa njia ya simu amekiri tukio la
mlio wa risasi kujitokeza katika ofisi za faraja, lakini mazingira yake hawezi
kuzungumzia hadi arudi ofisini, kwavile alikuwa safarini.
Hata hivyo Jonas Nkya alipopatikana amekanusha madai hayo na
kwamba kilichojitokeza ni kuanguka kwa bastola yake iliyokuwa kiunoni, baada ya
kwenda ofisi za faraja kubadilisha gari
kwaajili ya kwenda shamba, ambapo ilijifyetua risasi mbili na kutoa mlio
uliosababisha baadhi ya watu kusogea eneo hilo na kwamba kama kungekuwa na
ugomvi wa kifamilia, ungefanyika nyumbani kwao ambapo yupo kwa sasa, akimsaidia
mama yake kumuuguza baba yake Prof Nkya,ambaye amepooza, madai ambayo yameungwa
mkono na mama yake mzazi ambaye naye amehojiwa katika ofisi za faraja, baada ya
kukutwa akiendelea na majukumu yake.
No comments:
Post a Comment