Wafanyakazi kampuni inayomiliki lori hilo ambayo bado
haijafahamika, wakifanya tathmini ya hasara iliyopatikana
Lori likiwa limeteketea kabisa
LORI la mafuta aina ya Scania likiwa limesheheni dizeli
likitokea bandarini jijini Dar es Salaam kuelekea mikoani, liligonga tuta
katika Barabara ya Morogoro, eneo la Kimara-Baruti, likapoteza mwelekeo na kupinduka kisha kuwaka
moto na kuteketea kabisa.
Wakati lori hilo likiwaka, mafuta yenye moto yalisambaa na
kutaka kuunguza nyumba za jirani lakini Kikosi cha Uokoaji na Zima Moto cha
Halmashauri ya Jiji, kiliwahi kufika eneo la tukio na kuudhibiti moto huo.
Tukio hilo limesababisha usumbufu mkubwa kwa magari
yanayotumia njia hiyo kutokana na sehemu hiyo kupitika kwa shida.
(HABARI/PICHA : RICHARD BUKOS / GPL
No comments:
Post a Comment