Mtoto aliyekuwa akiishi katika mazingira ya umasikini katika
Nyumba ya kulea Watoto yatima nchini Thailand amefanya uamuzi wa kushangaza
alipokataa ombi la Nyota maarufu duniani Kim Kardashian kumuasili kuwa sehemu
ya familia yake.
Taarifa zinasema binti huyo alifurahi sana aliposikia
milionea huyo anataka kumuasili, lakini alisisitiza kuwa anataka kusoma nchini
Thailand akimtaka Kim kuisaidia nchi yake na watoto wenzake wanaoishi pamoja
katika nyumba ya watoto yatima.
Kim alivutiwa na binti huyu aitwae Pink mwenye umri wa miaka
13, alipotembelea nyumba ya watoto yatima katika Jimbo la Phang Nga,eneo ambalo
zaidi ya watu 4,000 walipoteza maisha kutokana na Tsunami mwaka 2004.
Pink alipelekwa na mama yake katika nyumba ya kulelea watoto
kwa kuwa hakuweza kumlea mtoto huyo na kugharamia elimu yake.
Binti huyu anasema yeye na Watoto wenzake walipokutana na
Kim Kardashian hawakumfahamu yeye ni nani.
Pink ambaye jina lake halisi ni Laddawan Tong-Keaw,
alifurahi kukutana na Nyota huyo, amesema na yeye anapenda sana kuonekana
kwenye Televisheni.
Pink husafiri umbali wa Maili 100 kwa basi na Watoto wenzake
wawili kwenda Shule inayoongoza jimboni humo inayomilikiwa na Serikali baada ya
kufaulu mitihani yao kuingia shule hiyo.
Binti huyu huamka saa kumi na moja alfajiri na kurejea
nyumbani saa kumi na mbili jioni.
No comments:
Post a Comment