Kama nikiwa bosi hautapata siku ya kupumzika, ndio maana mshahara umewekwa kwaajili yako ili kumpa mwajiri muda wa kutosha kuwa huru. Hutakiwi kumwomba bosi wako muda wa kupumzika wakati una muda ulishawekwa kwaajili yako. Muda mwingine uliobaki umebadirishana na mshahara.
2. Je ninaweza kwenda likizo?
Natumaini kuwa una siku zako ambazo zipo kwaajili yako. Hutakiwi kuuliza kama unatakiwa kwenda likizo au la unachotakiwa kufanya ni kutoa taarifa kuwa unakwenda likizo. Hutakiwi kuomba kitu ambacho ni haki yako kupata au kuwa nacho la unachotakiwa kufanya ni kutoa taarifa mapema ili watu wajue.
3. Je hatima yangu kwenye shirika hili ni ipi?
Bosi wako hawezi kukwambia kesho yako itakuwaje hata wao au yeye mwenyewe hajui kesho yake kwenye shirika hiyo ikoje sembuse kuhusu wewe?
4. Je ninaweza kuongezewa mshahara?
Kupandishwa mshahara au kupandishwa cheo ni vitu ambavyo unatakiwa ufanye kazi kwa juhudi ili uweze kustahili hayo. Hivyo unatakiwa kuonyesha umeweza kufanya ini au mafanikio yako yametoka wapi na umefika wapi.
6. Je waonaje kuhusu utendaji wangu?
Hili swali linamuacha bosi wako afikiri kuwa hujaridhika na nafasi uliyonayo kwenye ngazi uliyopo. Na pia inawezekana utendaji wako ni wa kusuasua. Kama utendaji wako sio mzuri utapata jibu litakalokukatisha tamaa.
7. Je ninaweza kufika kwa kuchelewa?
Kama kuna foleni unatakiwa kujua muda gani ni muafaka kutoka nyumbani kwako au kupeleka watoto wako shule. Hakuna asiyejua mjini kuna foleni hivyo hiyo sio dharula.
8. Je ninaweza kuondoka mapema?
Swali hili halina tofauti na swali lililopita, bosi wako hajali kama unawahi foleni hilo ni tatizo lako binafsi.
9. Je ulipata friend request yangu?
Usimtumie habari ya kuomba urafiki bosi wako kwenye Facebook, Twitter au mtandao wowote wa kijamii. Mitandao hiyo ni maisha yako binafsi na inatakiwa ibake hivyo. Bosi wako hatakiwi kujua kitu gani kinaendeleea kwenye maisha yako ya kawaida, umekula nini, umevaa nini mwisho wa wiki au ulikwenda wapi na vitu kama hivyo.
Linkedin ni mbaya kwa kuwa ni kama unataka kumfanya bosi wako ajue fursa gani zingine unazozifukuzia ni sawa sawa na kumuunganisha mkeo au mmeo kwenye match.com halafu awe rafiki yako huko.
10. Unatarajia kufanya nini wikiendi hii?
Huko ni kuvuka mipaka kati ya kazi na maisha binafsi na utamfanya aanze kukuchukulia kwa umakini mkubwa. Swali hili halina makosa ila inategemea unamuuliza nani? Atakavyolipokea ni tofauti na ulivyouliza. Kitu cha msingi inakubidi uangalie ni namna gani unauliza maswali kwa watu walio juu yako kabla ya kufanya makosa katika uulizaji wako.
No comments:
Post a Comment