nguo ya ndani inayoweza kuvaliwa na watu wa jinsia zote sasa
imeanza kuuzwa madukani nchini Marekani.
Hii ni baada ya kampuni moja nchini humo kuanza kutengeza
nguo za ndani kwa lengo la kuhakikisha kuwa wapenzi wanaweza kutumia nguo moja
bila tatizo lolote.
Kulingana na gazeti la the telegraph,nguo hizo kwa
jina Play
out zinazotengezwa na kampuni ya Abby Sugar na Sylvie Lardeux pia
zinashirikisha suruali fupi zenye rangi ya kung'aa.
nguo hizo zimetengezwa kama za kiume lakini hazina zipu
swala linalozifanya kuweza kuvaliwa na jinsia zote,ijapokuwa wengine wanaweza
kulalama kwamba haziwapi faraja.
''Tunataka watu wajisike vizuri na wawe wenye raha wakati
wanapovalia nguo hizi,lakini sio kuvaa ili kuwafurahisha watu wengine'',
alisema bi Sugar ambaye amekuwa na uhusiano na Bi Lardeux kwa kipindi cha miaka
mitano iliopita.
Wanasema kuwa waliamua kutengeza nguo hizo kwa kuwa wanaona
mtindo wa chupi za wanaume kama zinazofurahisha na kuvutia .CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment