Mchezaji wa Kimataifa wa Timu ya Taifa ya Uholanzi na Timu za Barcelona, AC Milan, Patrick Kluivert, akizungumza na Mkurugenzi wa Redio Coconut Ali Dai ambaye ndiye aliyesimamia safari ya Mchezaji huyo Zanzibar kupitia Kampuni ya TSN, iliodhamini safari yake hiyo Zanzibar, kwa ajili ya mapumziko na kutembelea sehemu za historia ya kisiwa cha marashi ya karafuu.
Mkurugenzi wa Redio Coconut FM Ali Dai akimtambulisha Mkurugenzi wa Coconut TV Ndg, Rashid Tamale wakati wa kumuaga Mchezaji wa Kimataifa wa Timu ya Taifa ya Uholanzi na Timu za Barcelona na AC Milan, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Mwakilishi wa Rahaleo na Mpenzi wa mchezo wa mpira wa miguu Zanzibar Mhe. Nassor Salim Jazira, akisalimiana na Kluivert uwanja wa ndege wakati wa kuondoka Zanzibar baada ya mapumziko yake ya siku nne katika moja ya hoteli za kitalii kiwengwa.
Waandishi wa habari wakimuhoji wakati akiwa katika harakati za kuondoka Zanzibar baada ya ziara yake ya mapumziko Zanzibar kwa siku nne.
No comments:
Post a Comment