Mwanamuziki mmoja mashuhuri wa miondoko ya Pop kutoka
Lebanon amekemewa katika mitandao ya kijamii na watu jamii ya waarabu wakiwemo
Wanawake.
Wiki iliyopita, muimbaji huyo Haifa Wehbe alitoa burudani ya
wimbo katika mashindano ya kipaji cha kuimba kinachorushwa na Televisheni cha
nyota wa kiarabu akiwa amevalia gauni refu jeusi lililomkamata barabara maungo
yake na linayomuonyesha sehemu za mwili wake.
Zaidi ya Watu milioni mbili walimuona mwanamuziki huyo
aliyekuwa jukwaani .Walitazama kwa njia ya Televisheni na intaneti baada ya
vipande vya video yake kuwekwa kwenye mtandao wa YouTube.
Watu waliguswa na video hizo hasa wanawake nchini Misri,
Jordan na Saudi Arabia, wakakemea vikali namna mwanamuziki huyo alivyochagua
mavazi yake.
Maoni kuhusu namna ambavyo mwanamke wa kiarabu anapaswa
kuvaa yalionekana kutawala zaidi, huku Lebanon mavazi mafupi ya kubana kwao si
hoja.
Katika nchi nyingine mfano Saudi Arabia, wanawake hujifunika
nyuso zao na miili yao kwa mavazi meusi , hata hivyo wanawake wamekuwa
wakiwafuatilia watu maarufu wakiwa katika hali ya kujificha au katika maeneo
wanapokusanyika wanawake peke yao.
Watu wengine wamesifu kile alichokivaa wakisema kila mtu ana
uhuru wa kuvaa atakacho, na si mara ya kwanza kwa watu kuvaa nguo zenye
kuonyesha maungo.
Dana Khairallah anamiliki blogu ya mitindo, haungi mkono
msimamo wa watu dhidi ya mwanamuziki huyo akisema kuwa haya yanakuja kwa sababu
ya uwepo wa mvutano kuhusu tamaduni za kiarabu wakidhani kuwa kuvaa hivyo ni
kuharibu utamaduni jambo ambalo amesema si kweli. Kisha akahoji kuwa huwa
anawaona wasichana wakiarabu wakiwa katika mavazi mafupi yenye kufedhehesha
katika kumbi za burudani nyakati za usiku lakini hakuna anayejali kwa kuwa
hakuna kamera.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment