Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, November 26, 2014

MWILI WA MPENDWA WETU SEBASTIAN MGIMBA WAPUMZISHWA KWA AMANI KATIKA MAKABURI YA KINONDONI

 Ndugu wa Marehemu Sebastian Mgimba Philipo Mgimba (katikati) akiwa amebeba msalaba huku pembeni ndugu mwingine akiwa pamoja na picha ya marehemu wakati wa misa fupi ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam leo.
Dada wa Marehemu Sebastian Mgimba, Mariam akiwa na ndugu zake wakati wa sala ya mazishi iliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni leo


 Rafiki wa Marehemu akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Sebastian Mgimba mara baada ya sala fupi ya mazishi kufanyika
 Baba Mzazi wa Marehemu Sebastian Mgimba, Mzee Mgimba pamoja na Mama wakiwa na shada la maua tayari kwa kuweka juu ya kaburi la Mtoto wao Marehemu Sebastian Mgimba
 Ndugu wa Marehemu Sebastian Mgimba wakiweka shada la Maua juu ya kaburi la Marehemu Sebastian Mgimba
 Dada wa Marehemu Sebastian Mgimba, Bi Mariam Lukaza akiwa na mumewe Johnson Lukaza wakijiandaa kuweka shada la Maua juu ya Kaburi la Marehemu Sebastian Mgimba katika mazishi yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar Es Salaam.
Mama Leoncia Lukaza akijiandaa kuweka Shada la Maua kwa niaba ya familia ya Lukaza katika kaburi la Marehemu Sebastian Mgimba kwenye mazishi ya marehemu Sebastiani Mgimba yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
Umati wa Watu waliojitokeza kwaajili ya Kumpumzisha Ndugu yetu Sebastian Mgimba katika makaburi ya Kinondoni.Picha na Josephat Lukaza - 
Marehemu Sebastian Mgimba alifariki dunia tarehe 20 Nov 2014 nchini Malaysia, Marehemu ameacha Mke na mtoto mmoja. Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi Amin

No comments:

Post a Comment