Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, November 23, 2014

Picha za Harusi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini David Kafulila

 Kwenye historia ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana kuna historia nyingine inaandikwa ambapo Mbunge mwingine amefunga Ndoa.
Tumezoea Wabunge wetu wakipewa nafasi ya kuchangia jambo ndani ya kikao cha Bunge huwa wanaanza kwa pongezi, utasikia hivi; “.. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge au Waziri………”
Jumatatu kikao cha Bunge kitaendelea na nadhani hautoshtuka ikitokea Mbunge hata mmoja akisema hivi; “… Nimpongeze sana Mheshimiwa David Kafulila, Mbunge wa Kigoma Kusini kwa kufunga ndoa siku ya Jumamosi..”
Yes.. Ni kweli.. Mbunge huyo amefunga ndoa leo Kigoma, ujumbe alioandika Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Facebook ni huu hapa; “..Bwana Harusi David Kafulila akiwa na msimamizi wa ndoa yake Deo Filikunjombe na marafiki zake David Silinde na Mwami..” halafu kuna picha aliyoiweka akiwa na Wabunge hao.





 Mbunge wa Kigoma Kusini Mhe David Kafulila akiwa na mai waifu wake Jessica Kishoa wakijiandaa kukata utepe wa kuingia katika mnuso kwenye ukumbi wa Annex uliopo Uvinza, Kigoma,  jana Jumamosi Novemba 22, 2014
 Mhe David Kafulila akiwa kanisani  na mai waifu wake wa Jessica Kishoa wakati wa  kufunga ndoa katika kanisa la Roman Catholic katika Parokia ya uvinza, Kigoma, jana Jumamosi Novemba 22, 2014
 Mhe David Kafulila na mai waifu wake Jessica Kishoa pamoja na wapambe wao Mhe. Deo Filikujombe na mke wake Sarah Filikunjombe wakipeleka keki kwa wazazi wa bwana harusi 
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge waliopamba  harusi ya Mhe. David Kafulila katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Mhe Deo Filikunjombe. Mhe.David Kafulila ambaye ndiye Bw. Harusi, Mhe  Zitto Kabwe na Mhe David  Silinde. Picha zote na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma

No comments:

Post a Comment