Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 20, 2014

STRAIKA YANGA ATANGAZA KWENDA STAND

                                                Mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi.
Martha Mboma na Saphyna Mlawa
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Said Bahanuzi, amefunguka kuwa, yupo tayari kwenda kuitumikia Stand United.
Mshambuliaji huyo amesema yeye hana kikwazo endapo tu timu hizo mbili zitakubaliana.
Straika huyo kwa sasa hana nafasi katika kikosi cha Yanga ambayo alijiunga nayo akitokea Mtibwa Sugar.
Akizungumza na Championi Jumatano, Bahanuzi alisema yupo tayari kwenda kuitumikia timu hiyo 


ingawa na yeye taarifa za kutakwa kwake amekuwa akizisikia katika vyombo vya habari tu.(P.T)
Straika huyo alisema kuwa si kwa Stand pekee, hata kama kuna timu nyingine itataka huduma yake isisite kukutana na uongozi wa timu yake ya sasa.“Nipo tayari kwenda kuitumikia Stand United na timu nyingine yoyote ambayo itanihitaji lakini kikubwa ni lazima waongee na kukubaliana na uongozi wa Yanga kwa sababu bado nina mkataba nao.

“Sibagui timu kwa sababu kikubwa ni kupata nafasi ya kucheza na kuendeleza kipaji changu na soka ndiyo ajira yangu kubwa,” alisema Bahanuzi.Ikumbukwe straika huyo mwaka 2012 alifanikiwa kuibuka mfungaji bora wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).

No comments:

Post a Comment