Watoto watatu kutoka kijiji cha Barca katika kaunti ndogo ya
Aber Wilayani Oyam nchini Uganda wameanza kuzungumza lugha tofauti isiojulikana
baada ya kufungiwa katika nyumba kwa miaka saba.
Lugha hiyo mpya imetajwa kuwa Leb -adam ikimaanisha lugha ya
ubongo na jamii ya eneo hilo.
Inadaiwa kuwa baba ya watoto hao aliwafungia ili kuwalinda
kutokana na hatari yoyote.
Kulingana ma gazeti la the monitor nchini Uganda,watoto hao
hawajaathirika kiakili lakini
hawawezi kuzungumza na watu wengine.Wanaamini tu
kile baba yao anachowaambia.
Kulingana na mama yao watoto hao waliweza kuishi kwa kula
mayai ya chura yaliochemshwa na majani,ambayo hula kila asubuhi na jioni na
hutumia maji kutoka shimo lililochimbwa na baba yao.
Mama yao anasema kuwa baba ya watoto hao alimzuia
kutozungumza nao hatua iliowafanya kutojifunza lugha ya kiluo wakati walipokuwa
wadogo.
Mwanamke huyo amesema kuwa alionywa na baba huyo kutosema
chochote kuhusu watoto hao.
No comments:
Post a Comment