George H.W Bush
Aliyekuwa rais wa Marekani
George H.W Bush amekimbizwa katika hospitali moja ya Houston nchini Marekani
baada ya kupatikana na tatizo la kupumua.
Kulingana na madaktari,Bush
mwenye umri wa miaka 90 anachunguzwa katika hospitali ya Methodist.
Alipelekwa katika hospitali hiyo
na ambalensi jumanne usiku.
Wawakilishi wa Bush wanasema
kuwa hatua hiyo ya kupelekwa hospitali ni kama tahadhari.
Rais huyo wa 41 ndio mzee kuwahi
kuiongoza Marekani akimshinda Jimmy Carter kwa miezi michache.
Alihudumu kwa muhula mmoja baada
ya kushindwa na Rais Bill Clinton.
Bush ambaye hawezi kutumia miguu
yake,hivi majuzi alionekana amekaa katika kiti cha magurudumo katika hafla
iliofanyika mwezi November katika chuo kikuu cha Texas na mwanawe aliyekuwa
rais George W Bush.
No comments:
Post a Comment